Rekodi za Soka Ambazo Hazijavunjwa

 Rekodi Za Soka Ambazo Bado Hazijavunjwa

Ni rahisi kusema kwamba rekodi ziliwekwa ili zivunjwe lakini inakuja shughuli kubwa mno kwenye kuzivunja baadhi ya rekodi. Leo nakuletea rekodi zilizowekwa na magwiji wa soka ulimwenguni ambazo pengine itapita miaka buku bila kuvunjwa.

 #1 Zinedine Zidane

Zidane hakuwahi kuripotiwa kuwa ameotea hadi amestaafu mpira. Licha ya kuwa mchezaji gwiji kweli kweli akikiwasha pale Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa lakini hajawahi kunaswa kwenye mtego wa kuotea katika maisha yake yote ya soka

 #2 Lahm 

Lahm (beki wa Bayern Munich) alicheza msimu mmoja na nusu bila kufanya madhambi kama mlinzi.

 #3 Rekodi ya Ground

Giroud alicheza dakika 90 kamili za mchezo bila kugusa mpira kwenye kombe la dunia la 2018.

 💥 Mlinda mlango aliyefunga mabao 128 katika maisha yake ya soka rekodi inashikiliwa Ceni wa Brazil.

 💥 Rekodi ya kadi nyekundu 36 katika mechi moja hii ilitokea Argentina.

 💥 Sadio Mane dakika 2 sekunde 56 hatrick.

 💥 Lewendoski mabao 5 ndani ya dakika 9 

 💥 Toni kroos alienda kwa dakika 1000 plus ambayo ni zaidi ya michezo 12 bila kupoteza pasi.

 💥 Kufunga mabao 105 katika mwaka wa kalenda rekodi hii inashikiliwa na Godfrey Chitalu wa Zambia lakini fifa hawakuweza kukiri kuwa wanakubali rekodi ya Messi kufunga mabao 91 ya kalenda.

 💥Real Madrid  Kuchukua ubingwa wa UCL mara 3 mfululizo .

 💥 Manchester United haijawahi kupoteza mchezo wa nyumbani wakati wa kusoma kipindi cha kwanza tangu 1984.

🔥 Arsenal kubeba ubingwa wa EPL kwa kucheza michezo 38 ya Ligi bila kufungwa

Endelea kufuatilia makala mengine motomoto ya kimichezo kupitia SokaVIP

 Ni rekodi ipi imetisha zaidi?

                                                                              #SokaVIP

*

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post