Simba na Kibu Kimeeleweka

Sakata la Simba na Kibu Limefikia Patamu

Sakata la mchezaji wa Simba, Kibu Denis (Kibu D, Mzee wa kuwakanda) na klabu yake halali ya Simba SC limefikia Patamu. 


Mchezaji Kibu D alipewa ruhusa ya kwenda mapumzikoni na kutimkia nchini Marekani na picha pia zilimwomesha akiwa USA. Lakini klabu ilipomuhitaji kujiunga na wenzake hakutoa maelezo kamili au ya kueleweka, ikafahamika kuwa yupo nchini Norway akipatiwa vipimo Kwa ajili ya kulamba dili nono la kuichezea klabu mojawapo nchini humo. 
Inasemekana mambo yote yamekwenda sawia isipokuwa hawezi kusaini mkataba na klabu yoyote ikiwa yeye ni mchezaji halali wa Simba kimkataba.
Kwa sasa iko wazi kwamba ili Kibu afanikishe mipango yake, hana budu kurudi Kwa unyenyekevu mkubwa kuomba msamaha Kwa uongozi wa Simba na kuomba busara zao za kuvunja mkataba kama mkataba wao unavunjika. 

*

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post