Jinsi ya kuedit / kurekebisha nakala Ajira Portal

 Jinsi ya kuedit / kurekebisha nakala Ajira Portal – Utumishi

Leo kutoka Utumishi, Jinsi ya kubadili taarifa ajiraportal – Jinsi ya kufuta cheti, document yoyote ile Jinsi ya kuedit / kurekebisha nakala Ajira Portal; Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 iliyorejewa 2019, ambayo inaelekeza kuwepo kwa chombo maalumu cha kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Jukumu la msingi la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni kuwezesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Idara na Taasisi mbalimbali za Umma.

Hivi karibuni zimetangazwa nafasi za kazi mbalimbali na watanzania wenye sifa wanatakiwa kuomba nafasi hizo kupitia mfumo wa Ajira Portal. Katika mfumo huu muombaji kazi anatakiwa kupakia nakala za vyeti vyake ambazo zimehakikiwa na kugongwa mhuri na Mwanasheria au Wakili kuonesha kuwa ni nakala kutoka katika vyeti halisi.

Pia Muomba kazi anatakiwa kupakia vyeti vyake kwenye mfumo kulingana na kiwango chake cha elimu ili kumuwezesha kuomba pindi nafasi zinapo tangazwa. Ikitokea umeudanganya mfumo au umeweka cheti cha taaluma kisicho cha kwako, au unataka kuomba nafasi ya juu au ya chini kulinganisha na cheti cha taaluma ulichonacho, hutoweza kuomba nafasi uliyoomba kwani mfumo unamtambua cheti chako cha elimu ambacho umeweka kwenye mfumo.

Ikitokea umekosea kupakia cheti chako, Mfumo hauto kuruhusu kufuta cheti chako bali utalazimika kwenda sehemu uliyo kosea na kuhariri (edit) cheti chako kisha kupakia (upload) kilicho sahihi.

Hata hivyo; Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetambua changamoto wanazokutana nazo waombaji kazi na imeweka simu ya Huduma kwa mteja namba 0262160350 inayopatikana kuanzia saa 2.00 Asubuhi mpaka saa 12.00 Jioni kwa siku za kazi na Maafisa wapo tayari kwa ajili ya kutoa huduma au unaweza kutuma barua kupitia ict@ajira.go.tz

*

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post