Maana Halisi ya Kariakoo

 Je, Unaijua Maana ya Jina Kariakoo?

Kila jina sehemu lilikuwa na/lina maana yake na chanzo Cha kupewa jina hilo. Mara nyingi majina ya sehemu hutokana na shughuli zinazofanyika mahali hapo, kitu maarufu kilichopo au utata wa matamshi ya maneno nk.


Unaweza kujiuliza jina la kata ya Kariakoo sehemu ya kibiashara iliyopo Wilaya ya Ilala Jiji la Dar es Salaam lilipatikanaje na lina maana gani. Unaweza kuhisi pengine linatokana na muunganiko wa maneno mawili "Karia" (kukaria) na "koo" na kupata neno "Kariakoo" (Kukaria kooni) lakini siyo kweli. 
Leo nimeona nichimbe na kutafuta maana halisi ya neno hili na lilipatikanaje.

Asili ya neno Kariakoo

Wakati wa vita vya Kwanza vya Dunia, Uingereza ilipigana na Ujerumani hapa Afrika Mashariki. Baada ya vita kupamba moto uhitaji wa askari uliongezeka, Uingereza alitumia askari ya Kihindi kama askari wa nje na kuwaacha Machifu kutekeleza majukumu ya ulinzi wa ndani katika ufanisi mdogo.
Gharama ya kuwahudumia askari wake na askari wa Kihindi hasa Kwa upande wa chakula ilikuwa kubwa kwani kufikisha kilo moja ya Michele iligharimu kula kilo 50 za Michele njiani. Hivyo, wakaamua kuunda kikosi Cha askari kutoka Kwa waafrika wenye huku huku Afrika Mashariki (programu ilianzishwa Kenya). Kikosi Cha takribani askari wa kiafrika 400,000 kiliundwa. Kikosi hicho kilijulikana kama Carrier Corps (Karia Kops) yaani kikosi Cha askari.
Kwahiyo, askari hao wa kiafrika wakaanza kupigana na wazungu na kuwaamusha waafrika na viongozi wa kisiasa wa Afrika kuona kumbe wazungu wanakufa tena kuuliwa na waafrika, hii iliwapa motisha ya kuanza kupigana Kwa maslahi yao.
Baada ya vita vya Kwanza askari kutoka carrier corps walipewa maeneo ya kuishi, maneo hayo ni Kariakoo, Dar es Salaam, Kariakor ya Nairobi, Kariakor ya Zambia na Kariakor ya Voi.
Maeneo haya yaliitwa Kariakoo/Kariakor kutokana na kuishi Kwa hawa Carrier Corps. 

Tuandikie kwenye comment maana ya Kariakoo uliyokuwa nayo kichwani kabla ya kusoma makala hii.


Kama umependezwa na makala hii tafadhali tusaidie kuisambaza mitandao ya kijamii

*

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post