Dereva Daraja II - Ajira 1
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti anapenda kuwatangazia nafasi ya kazi kwa madereva wenye ufaulu na uzoefu wa udereva daraja la II.Wajibu na Majukum
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kufanya usafi wa gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Elimu na Uzoefu:
- Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
- Awe na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Kima cha Mshahara: TGS B
💥Matangazo 🎄